Fomu Ya Ushiriki Wa Tuzo Za Vinara Katika Kupambana Na Ukatili Wa Kijinsia (GBV) 2023

WiLDAF pamoja na Mtandao wa Kupambana na Ukatili wa Kijinsia (MKUKI) wanaandaa Tuzo za Vinara wa Kupambana Dhidi ya Ukatili wa Kijinsia ikiwa ni sehemu ya Kampeni ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia. Hii ni katika kutambua na kupongeza juhudi za watu binafsi na mashirika ambayo yamechukua hatua kubwa na za kipekee katika kukomesha vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii zao na Tanzania kwa ujumla.

Hivyo basi, tunaomba ushiriki wako kwenye zoezi hili kwa kujaza fomu hii na kuweka mapendekezo ya vinara wanaostahili kuchukua tuzo katika vipengele vifuatavyo;