skip to Main Content

*Chukua tahadhari dhidi ya COVID-19.* 

Unaweza kupunguza nafasi ya kuambukizwa na kuenea kwa virusi vya Corona-19 kwa kuchukua TAHADHARI zifuatazo,

  1. Safisha mikono yako Kwa sabuni na maji tiririka mara kwa mara.
  2. Kaa umbali wa mita 1(hatua 3) baina yako na mtu mwingine.
  3. Epuka kwenda sehemu za mikusanyiko.
  4. Epuka safari zisizo za lazima.
  5. Epuka kugusa macho, pua na mdomo.
  6. Funika mdomo wako na pua kwa sehemu ya ndani ya kiwiko cha mkono wako, kitambaa safi au tishu wakati unapo piga chafya au kukohoa.
  7. Jitenge na kaa nyumbani hata pale utakapo onyesha dalili ndogo Kama kikohozi, maumivu ya kichwa, homa kali na kupumua kwa shida mpaka pale utakapo pona. Ikikulazimu kutoka nyumbani vaa barakoa ili kuzuia kuambukiza wengine.
  8. Ikiwa una homa, kikohozi na kupumua kwa shida toa taarifa kwa mamlaka husika au muone daktari.
  9. Endelea kufuatilia taarifa kuhusu maambukizi ya virusi vya corona na njia za kujikinga kutoka kwa vyanzo vya kuaminika.
  10. Kujua zaidi kuhusu Corona piga namba 08001100124 au 199 au *199# bure kwa Tanzania

Jikinge na wakinge wengine Corona inazuilika

Kiunga Kingine:

World Health Organization (WHO)

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto 

Back To Top