skip to Main Content

International Women’s Day 8th March 2018

SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

KIPUNGUNI, ILALA

TAREHE 08 MACHI 2018 

Kwa niaba ya wanachama wa Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Afrika, (WiLDAF Tanzania) na kwa niaba ya Mtandao wa Kupambana na Ukatili wa Kijinsia (MKUKI) tukishirikiana na Wasaidizi wa Kisheria Kipunguni tunayo furaha kubwa kujumuika na wanajamii wa Kipunguni kusheherekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

Mwaka huu Maadhimisho ya Siku ya Mwanamke Duniani kauli mbiu ni:

“Kuelekea Uchumi wa Viwanda, Tuimarishe Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji Wanawake Vijijini”

Kauli mbiu hii inatukumbusha na inataka wanawake hata walioko vijijini kuweza kufikia hatua nzuri ya uzalishaji tukiwa tunazingatia maswala mazima ya jinsia hasa katika kupiga vita na kutokomeza matendo ya ukatili wa kijinsia.

Ndugu Mgeni Rasmi;

WiLDAF kwa kushirikiana na Wasaidizi wa Kisheria Kipunguni tunaunga mkono nia ya Rais Dr. John Magufuli kuona Tanzania ya viwanda hasa kwa kupambana na matendo ya ukatili ikiwemo ukeketaji kusudi wanawake nao waweze kushiriki kikamilifu katika kuelekea uchumi wa viwanda.

Sanjari na hilo, WiLDAF pamoja na Wasaidizi wa Kisheria Kipunguni tunasheherekea maadhimisho haya katika jamii yetu ya hapa Kipunguni kwa kauli mbiu isemayo:

“Hakeketwi Mtu 2018”

  1. Kauli mbiu hii inatukumbusha sisi sote kama Jamii kwa nafasi zetu kuwajibika katika kuzuia na kutokomeza vitendo vyote vya ukatili wa Kijinsia ikiwa ni pamoja na suala la ukeketaji kwani madhara yake ni makubwa na yanamgusa karibu kila mtu kwa namna moja au nyingine, kuanzia ngazi ya familia, jamii na taifa kwa ujumla. Na ndio sababu tunasema “Hakeketwi Mtu 2018”. Hivyo basi ni jukumu la kila mmoja wetu “kuchukua hatua” kwa kupinga vitendo vya Ukeketaji na vitendo vyote vya ukatili wa kijinsia katika jamii zetu.

This Post Has 0 Comments

Leave a Reply

Back To Top