Wanawake Sasa - Ziara kwa Vyama vya Siasa

Katika kuadhimisha Mwezi wa Wanawake Duniani, WiLDAF kwa kushirikiana na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa tunaendelea kuhakikisha mazingira rafiki kwa ushiriki wa wanawake katika siasa. Tumeshatembelea vyama mbalimbali kukusanya maoni kuhusu rasimu ya mwongozo wa kutengeneza sera ya jinsia na mwongozo wa uundaji na uendeshaji wa dawati la jinsia katika vyama vya siasa.
Hii ni hatua muhimu katika kujenga mifumo jumuishi inayowezesha wanawake kushiriki na kuongoza kwa usawa katika uwanja wa siasa!
Mifumo bora yenye kumkinga mwanamke na aina zote za ukatili itasaidia kuongeza ushiriki wa wanawake wenye sifa kwenye ngazi za uongozi na maamuzi.

In celebrating International Women’s Month, WiLDAF, in collaboration with the Office of the Registrar of Political Parties, continues to ensure a conducive environment for women’s participation in politics. We have visited various political parties to collect feedback on the draft gender policy framework and guidelines for establishing and managing gender desks within political parties.

This is an important step in building inclusive systems that empower women to participate and lead equally in the political arena!

Well-structured systems that protect women from all forms of violence will help increase the participation of qualified women at leadership and decision-making levels.