Her Story Journal 2 Launch:
1. Mungu Ibariki Afrika, (God Bless Africa)
Wabariki Viongozi Wake, (bless her leaders)
Hekima, Umoja na Amani (wisdom, unity and peace)
Hizi ni Ngao Zetu,(these are our shields)
Afrika na Watu Wake. (Africa and her people)
Ibariki, Afrika, (Bless,Africa)
Ibariki, Afrika, (Bless,Africa)
Tubariki, Watoto wa Afrika,(Bless, Children of Africa)
2. Mungu Ibariki Tanzania, (God Bless Tanzania)
Dumisha Uhuru na Umoja,(sustain independence and unity)
Wake kwa Waume na Watoto,(Women, Men and Children)
Mungu, Ibariki, (God, Bless,)
Tanzania na Watu Wake (Tanzania and her people)
Ibariki, Tanzania, (Bless,Tanzania)
Ibariki, Tanzania, (Bless,Tanzania)
Tubariki, Watoto wa Tanzania (Bless, Children of Tanzania)
1. Ee Mungu twaomba uilinde
Jumuiya Afrika Mashariki
Tuwezeshe kuishi kwa amani
Tutimize na malengo yetu.
Chorus
Jumuiya Yetu sote tuilinde
Tuwajibike tuimarike
Umoja wetu ni nguzo yetu
Idumu Jumuiya yetu.
2. Uzalendo pia mshikamano
Viwe msingi wa Umoja wetu
Natulinde Uhuru na Amani
Mila zetu na desturi zetu.
3. Viwandani na hata mashambani
Tufanye kazi sote kwa makini
Tujitoe kwa hali na mali
Tuijenge Jumuiya bora.