Inatoa njia rahisi na ya siri ya kuwasilisha malalamiko ya ukatili wa kijinsia au wa aina nyinginezo. Unaweza kutoa taarifa kupitia ujumbe au kurekodi sauti.
Inajumuisha maktaba ya maarifa inayomsaidia mtumiaji kuelewa haki zake za kisheria na taratibu za kufuata pindi anapokumbana na changamoto mbalimbali.
Funguka App inawashirikisha wanaume kuwa washirika katika kuendeleza uongozi wa wanawake, usawa wa kijinsia, ulinzi, na ushiriki sawa katika kufanya maamuzi, pamoja na kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na wasichana.