skip to Main Content

Tamko Kupinga Udhalilishaji wa Viongozi Wanawake kwa njia ya Mitandao ya Kijamii

Mtandao wa Kupambana na Ukatili wa Kijinsia (MKUKI), ukiratibiwa na Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WiLDAF) unatoa pongezi za dhati kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa uteuzi  na mabadiliko ya viongozi wa Wizara, Mikoa na Wilaya uliofanywa Jumamosi tarehe 28/07/2018. MKUKI umefarijika sana na uteuzi huo kwani umezingatia vigezo vyote muhimu ikiwemo taaluma, ueledi, uwakilishi wa makundi ya rika mbalimbali ,uzoefu na usawa wa kijinsia.

Sisi MKUKI,  tumekuwa tukipigania usawa wa kijinsia katika ngazi  za kutoa maamuzi ili kuleta usawa wa kijinsia baina ya wanawake na wanaume.  Tunatambua jitihada za Mhe. Rais wetu katika kuhakikisha wanawake wanakuwa sehemu ya wafanya maamuzi. Katika teuzi hizo tumeona wanawake 10 wameteuliwa kuwa wakuu wa wilaya kati ya 31 na 2 wameteuliwa kuwa makatibu Tawala kati ya 13.

Kwa kipekee, MKUKI tunapenda kuwapongeza wanawake hawa malkia na vinara ambao jamii na vyombo vya uteuzi vimetambua talanta, uwezo na ujuzi wao. Tunaamini kuwa uteuzi wa uongozi umezingatia ueledi na uwezo wa kitaalamu sifa ambazo viongozi wateule wanazo.  Miongoni mwao viongozi hawa wateule wameishawahi kuwa mameneja wa kampeni katika umri mdogo, wajasiriamali na tena kupewa tuzo na jarida la Forbes chini ya miaka 30 katika bara la Afrika. Watu kama hawa wamekuwa mfano wa kuigwa miongoni mwa vijana, wanawake na watoto.

Hata hivyo,  MKUKI unasikitishwa na kulaani vitendo vinavyoendelea vya udhalilishaji na lugha za matusi  vinavyofanywa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii hapa nchini vikilenga kudhalilisha na kudhihaki, viongozi wanawake wateule hususan Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Bi. Joketi Mwegelo. Vitendo hivyo havikubaliki kwani ni ukatili mkubwa wa kijinsia na kinyume za haki za binadamu. Vitendo hivi vinadhalilisha wanawake wote, vinaingilia uhuru wa

 

mtu binafsi na vinaleta chuki baina ya jamii zetu. Ikumbukwe kuwa Sheria ya Mtandao Namba 14 ya Mwaka 2015 Kifungu cha 23 (1) & (2) inakataza mtu yeyote kutumia mtandao kuonea, kutishia, kudhalilisha au kumdhoofisha kihisia na kumsababishia huzuni mtu mwingine(cyber bullying).

Tunawaasa wanajamii kutotumia vibaya mitandao ya kijamii katika kudhihaki au kumdhalilisha Mhe. Jokate na viongozi wengine wote wa serikali na taasisi binafsi. Katiba ya Jamhuri ya Muungano inampa kila mtu haki ya kutoa maoni bila kuathiri haki ya mtu mwingine. Aidha ibara ya 12-(1) na (2) inatambua heshima na thamani ya utu pamoja na usawa na haki bila ubaguzi wowote.

Tunatoa wito kwa vyombo na mamlaka husika ikiwemo Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi na kubaini wahusika ili sheria ichukue mkondo wake kukomesha vitendo vya udhalilishaji dhidi ya wanawake , hususan kwa viongozi wetu.

Tunawatakia kila la kheri wanawake wote walioteuliwa katika nafasi hizi adhimu walizozipata kuwatumikia wananchi katika kuleta maendeleo na kukabiliana na changamoto mbalimbali za kijamii, kiuchumi na kiutendaji.

Imeandaliwa na:

1 Women in Law and Development in Africa (WiLDAF) Dar es salaam
2 Legal and Human Rights Centre (LHRC) Dar es salaam
3 Tanzania Gender Network Program (TGNP) Dar es salaam
4 Tanzania Women’s Lawyers Association (TAWLA) Dar es salaam
5 Women Legal Aid Centre (WLAC) Dar es salaam
6 Child Dignity Forum (CDF) Dar es salaam
7 Tanzania Media Women Association (TAMWA) Dar es salaam
8 Tanzania Network for Legal Aids Provider (TANLAP) Dar es salaam
9 Kivulini Women’s Rights Organization Mwanza
10 Centre for Women  and Children Assistance (CWCA) Mara
11 Taasisi ya Haki za Wanawake (HAWA) Dar es salaam
12 Word Vision Tanzania Dar es Salaam
13 Kilimanjaro Women Information Exchange and Community Organization (KWIECO) Kilimanjaro
14 Organization for Women Empowerment (OWE) Lindi
15 Agape Foundation Shinyanga
16 Tanzania Women and Children Welfare Centre (TWCWC) Dar es salaam
17 Gender Centre Dar es salaam
18 Anti-Female Genital Mutilation (AFNET) Dodoma
19 Wanawake katika Jitihada za Kimaendeleo (WAJIKI) Dar es salaam
20 Young Lawyers Foundation Dar es salaam
21 Women Action Towards Economic Development (WATED) Dar es salaam
22 Umoja wa WanawakeWanasiasa Tanzania (ULINGO) Dar es salaam
23 Dignity Kwanza- Community Solutions Dar es salaam
24 Chama cha Wajane Tanzania (TAWIA) Dar es salaam
25 Women Fighting Aids in Tanzania (WOFATA) Dar es salaam
26 Kikundi cha WanawakeWajasiriamali (ASE) Dar es salaam
27 TLD Dar es salaam
28 Centre against Gender Based Violence (CA-GBV) Dar es salaam
29 Tanzania Women’s Cross Party Platform (TWCP) Dar es salaam
30 Young Women’s Christian Association (YWCA) Dar es salaam
31 EKAMA Foundation Dar es salaam
32 LASEHA Dar es salaam
33 AWWOR Dar es salaam
34 Kigogo Youth Organization (KYO) Dar es salaam
35 Gender Media of Southern Africa Tanzania (GEMSAT) Dar es salaam
36 Zamzam Women Development (ZAWODE) Dar es salaam
37 VICOBA Kigamboni Dar es salaam
38 Network against Female Genital Mutilation (NAFGEM) Kilimanjaro
39 National Network in Tanzania Women with HIV/AIDS (NETWO+) Dar es salaam
40 Lindi Women’s Paralegal Aid Centre (LIWOPAC) Dar es salaam
41 Action for Justice for Society Tanzania (AJISO) Dar es salaam
42 New Hope New Winner’s Foundation Dar es salaam
43 Tanzania Women of Impact Foundation (TAWIF) Dar es salaam
44 Songea Paralegal Centre (SOPCE) Songea
45 Wasaidizi wa KisheriaMtwara Mtwara
46 Wasaidizi wa KisheriaTanga Tanga
47 Wasaidizi wa KisheriaBahi (SULUNGAI) Dodoma
48 Wasaidizi wa KisheriaKongwa (MWITAZAJE) Dodoma
49 Wasaidizi wa KisheriaRungwe (WAKIRU) Mbeya
50 Wasaidizi wa KisheriaKipunguni (Sauti ya Jamii) Dar es Salaam
51 Education Centre for the Advancement of Women Tanzania Dar es Salaam
52 Equality for Growth Dar es Salaam
53 Women Fund Tanzania Dar es Salaam
54 Women Wake-up (WOWAP) Dodoma
55 Mwezeshe Mama Dar es Salaam

AHSANTE

This Post Has 0 Comments

Leave a Reply

Back To Top